Klabu ya Manchester United ya Uingereza leo May 30 2016 imetangaza maamuzi mapya ambayo yatawapa furaha mashabiki wa klabu hiyo, Man United leo May 30 imetangaza kumpa mkataba wa miaka minne kinda aliyekuja kwa kasi Marcus Rashford.
Man United wamempa mkataba huo wa miaka minne utakamuoweka staa huyo Old Trafford hadi June 2020, Rashford mara ya kwanza kucheza mechi na kikosi cha kwanza cha Man United alifunga magoli mawili katika mchezo dhidi ya Midtjylland mwezi February.
Kinda huyo wa Man United amefanikiwa kumaliza msimu wa 2015/2016 akiifungia Man United jumla ya magoli 8 katika mechi 18 alizoichezea klabu hiyo msimu huu, Rashford kwa sasa ana umri wa miaka 18 na alianza kuichezea timu ya vijana ya Man United toka mwaka 2005, kinda huyo pia ameitwa katika kikosi cha England cha wachezaji 26 watakaoshiriki michuano ya Euro 2016.
No comments:
Post a Comment