Tuesday, 17 May 2016

kwanini mahusiano yanayodumu uanzia kwenye urafiki

Je…. Wewe una rafiki wa karibu (Best Friend) wa jinsia tofauti na wewe?  Basi hii ni kwaajiri yako.
Watu wengi husema hakuna urafiki kati ya mwanamke na mwanaume, yaani ni kama kufananisha urafiki wa Simba na Nyumbu ambao ni urafiki wa kinafki. Inaweza ikawa kweli lakini Kuna mambo kila mtu anatakiwa ajue, tunafahamu mahusiano mazuri ni yale ya watu wanaofahamiana kiundani, na mara nyingi marafiki wanaoshibana kwa dhati ni raisi kufahamiana Tabia na mambo mengine mengi.
watu wengi huogopa kuwa na mahusiano Na marafiki zao sababu ikitokea wakaachana au kugombana kama wapenzi basi  mapenzi yataisha na urafiki unaisha pia Lakini kama uhusiano huo ukienda vizuri  ni moja kati ya mahusiano ambayo hudumu kwa muda mrefu. Je  unajua ni kwanini?

Kumbukumbu MbaliMbali za Matukio Yenu pamoja.  

o-MICHELLE-OBAMA-900
Mambo mliowahi fanya kama marafiki huwa kumbukumbu nzuri katika maisha yenu ya mahusiano kwani hii inawafanya kuwa karibu na kujenga mahusiano imara  zaidi . maisha ya kula wote miogo vibandani michongo mliofanya pamoja na vituko kibao mlivyofanya pamoja, Kama ni wakati mkiwa shule au chuo. Kila kumbukumbu ni hazina.
kuwajua Familia na watu wa karibu.
epa03308465 US President Barack Obama (C) does a little dance while First Lady Michelle Obama (L) and the President's daughter Malia(R) look on as they attend an exhibition basketball game between the USA and Brazil at the Verizon Center in Washington DC, USA, 16 July 2012. The President is back on the campaign trail on 17 July with a day-trip to Texas.  EPA/JIM LO SCALZO

Watu uingia katika mahusiano na baadae ndio wanaanza kutambulishana  kwa familia lakini marafiki huwa huru kuwa na familia za marafiki zao na pindi watakapo anza mahusiano inakuwa raisi zaidi  kutambua wako na watu wa aina gani na hii pia hujenga imani kwa familia sababu  tayari unafahamika na familia hiyo hasa kitabia.
Rafiki ni msaada baada ya maumivu
michelle-obama-barack-obama-inline
 mara nyingi mtu akiumizwa katika mahusiano mtu wake wa karibu huwa rafiki na kwa watu ambao ni marafiki wa karibu (Best Friends)  huambiana mambo mengi ya moyoni ha hii hujenga kuaminiana  kwa  kiasi kwamba wanapokuwa katika mahusiano watu hawa hawatakuwa na wasiwasi juu ya kuaminiana sababu wameshakuwa pamoja wameshapitia maumivu na furaha pamoja kwahiyo mahusiano huzidi kuwa imara.
Siri zenu
barack_michelle

 Rafiki yako ni msiri wako marafiki wa karibu hujuana kiundani na hata kuambiana habari za siri. Mambo ya familia, uchumi,elimu hata afya  kitendo cha kubebeana siri zenu kama Marafiki pia ni rahisi kubeba mizigo na maumivu ya mwingine kwenye mahusiano na hata ndoa. Kuna baadhi ya watu wana tabia zao ambazo marafiki zao tu wa karibu ndio wanafahamu hata familia yake haitambui.
kila mtu yuko huru na mwenzake
huru


kitu kingine ambacho hufanya mahusiano ya aina hii kudumu ni uhuru kwani kila mmoja anakuwa kamzoea mwenzake kutoka zamani kwahiyo kila mtu anakuwa huru karibu ya mwenzake. Huwezi kuwaza uvae nini au uwe mtu wa aina gani mbele yake bali utakuwa kama wewe, na utakuwa huru sababu wewe ni rafiki. Na ukiweza kuwa mpenzi basi hakuna kitakacho badilika.
Mnaweza ongelea mahusiono yenu na watu wengine.
wengine

  Kwa marafiki  wa karibu kuongelea mahusiano yao ya mapenzi ni kawaida na hii kuwafanya kujuana kiundani  nini wanakikosa hasa wakiwa na mahusiano na watu wengine ni nini wanahitaji kama wapenzi na hii hufanya wao wajifunze kupitia wengine kuwa karibu. Mahusiano yao ya nyuma yanaweza wasaidia wao kujenga mahusiano yao imara kwa kujadili waliopitia kwa uhuru.  Tofauti na mtu usie mfahamu vizuri sio raisi kuyaongelea mambo ya mpenzi wake au wako wa zamani (ex).
 Rafiki anapokuwa kama mmoja wa familia. 
enhanced-buzz-wide-30160-1352326732-3
Rafiki ambae unaweza mkaribisha nyumbani katika matukio muhimu ya familia yako kama Harusi,/Msiba ni rafiki ambae ukiwa na mahusiano nae hawi mgeni kwa familia yako wala ndugu zako. Na kama mkiwa katika mahusiano haitokuwa shida kutambua mashemeji au mawifi sababu watu wengi hugombana na kuchukiana sababu hawajuani vizuri.
 kutambuana Udhaifu wenu. 
puppy 

Rafiki yako wa karibu anaweza jua udhaifu wako anaweza jua nini cha kukusaidia, hapa mnaweza kufika mbali hata katika mahusiano kwa sababu ya kuweza kuvumiliana mapungufu yenu na hii ni moja kati ya mambo watu wakiwa kwenye mahusiano wanashindwa, kama mkiweza katika urafiki mkiwa katika mahusiano mnaweza kudumu na kujua kukabiliana na hayo yote.
Kitu cha muhimu ni vyema kujadili mahusiano kabla hamjaanza hasa kama mmoja hayupo tayari kwani sio kila marafiki wa karibu uishia katika mahusiano ya kimapenzi kwani unaweza ukakuta hisia zako za mapenzi ni tofauti na mwenzako, hii ni kwa kulinda urafiki wenu kwani kama mnaingia kwenye mahusiano kwa sababu tu mmezoeana mahusiano hayo yanaweza yakaisha vibaya.

No comments:

Post a Comment