Tuesday, 17 May 2016

HAWA NDIYO WACHEZAJI WALIYO ACHWA KIKOSI CHA TAIFA CHA HISPANIA



Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa, kiungo wa Manchester United Juan Mata na mshambuliaji wa Atletico Madrid Fernando Torres wameachwa katika kikosi cha Spain kitakachocheza Euro 2016. Meneja wa Chelsea Guus Hiddink alisema mwishoni mwa wiki kuwa Costa huenda akakosa michuano hiyo kutokana na jeraha la msuli wa paja. Kiungo wa Atletico Madrid Saul Niguez ametajwa katika kikosi hicho. Spain wako kundi D, pamoja na Croatia, Jamhuri ya Czech, na Uturuki.

No comments:

Post a Comment