Wednesday, 30 March 2016

YANGA SC, AZAM FC, UWANJANI KESHO KUSAKA TIKETI YA CAF

Mechi ilianza vizuri lakini kadiri muda ulivyokwenda ndivyo mambo yalivyochacha
Mechi ilianza vizuri lakini kadiri muda ulivyokwenda ndivyo mambo yalivyochacha
Na Baraka Mbolembole
Wawakilishi pekee wa Tanzania waliosalia katika michuano ya Afrika, timu za Yanga SC na Azam FC siku ya kesho Alhamis watashuka dimbani kucheza michezo yao ya robo fainali katika kombe la FA. Baada ya timu mbili za visiwani Zanzibar kuondolewa katika michuano ya CAF, Yanga na Azam FC pekee ndiyo zimesalia.
Mafunzo iliondolewa hatua ya awali na AS Vita Club ya DR Congo katika hatua ya awali ya michuano ya klabu bingwa, wakati JKU yenyewe iliondolewa katika hatua ya pili ya michuano ya kombe la Shirikisho na waganda, Sports Club Villa.
Yanga itacheza na Ndanda kutoka Mtwara katika uwanja wa taifa wakati Azam FC itawavaa Tanzania Prisons ya Mbeya katika uwanja wa Azam Complex Chamanzi. Mshindi wa michuano hiyo ataiwakilisha Tanzania Bara katika michuano ya kombe la Shirikisho la Afrika baadaye mwakani.
Timu ya Mwadui FC ya mkoani Shinyanga tayari imefuzu kwa hatua ya nusu fainali baada ya kuiondoa Geita Gold Sports kwa kuitandika magoli 3-0 katika mchezo wa kwanza wa robo fainali wiki iliyopita. Mechi nyingine ya michuano hiyo itawakutanisha Simba SC na Coastal Union ya Tanga mchezo ambao pia utafanyika katika uwanja wa taifa, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki hii.
Yanga na Azam zimelalamikia ratiba ya kucheza mechi tano ndani ya wiki mbili wakati pia wakijiandaa kwa mechi dhidi ya timu kubwa za Afrika katika michuano ya CAF. Yanga itacheza na Al Ahly ya Misri katika ligi ya mabingwa wakati Azam itaivaa Esparance ya Tunisia.

No comments:

Post a Comment