Jina linalotajwa sana kurithi mikoba ya LVG ni Jose
Mourihno na kinachosubiriwa sasa hivi ni kutangazwa rasmi mwisho mwa
msimu huu kama mambo yakienda kama inavyodhaniwa.
Licha ya kuwa na perfomance mbovu akiwa anaiongoza club ya
Manchester United, lakini LVG hawezi kusahaulika kwa kitu alichofanya
ambacho ni kuwapa nafasi vijana kutoka kwenye academy ya Manchester
United.
Ryan Giggs amefurahishwa na kitu hicho na kusema maneno
ambayo ni kama onyo kwa kocha anayekuja Manchester United kuchukua kazi
ya LVG. Giggs amesema, “Hii imekua ni sehemu ya historia ya timu
yetu. Tofauti na club nyingine hapa tuna utaratibu kwa kukuza wachezaji
wetu na kuwa wachezaji wa kiwango cha dunia. Japokua tunaweza kuleta
wachezaji wa level hiyo lakini lazima tuwe na foward, winger au hata
beki ambae ana kiwango cha dunia na ametokea hapa hapa Manchester.
Mashabiki wanapenda na wanataka kuona wachezaji wanapitia katika njia
hii ya kwetu na wanaipa heshima yake. Hivyo basi watoto hawatakiwi
kusahaulika kwenye mfumo wa timu”.
Rashford ni mmoja kati ya wachezaji walipitia kwenye system hii na kuonyesha mafanikio makubwa.
No comments:
Post a Comment