BAADA ya Juzi kujigamba kwa kuwafunga Mabingwa wa Dunia Germany kwao Olympiastadion Jijini Berlin Nchini Germany katika Mechi ya Kimataifa ya Kirafiki kwa kuitandika 3-2, England Jana walirudishwa pale walipozoea kwa kuchapwa 2-1 Uwanjani kwao Wembley na Netherlands.
Netherlands, ambao Juzi walichapwa 3-2 na France, Jana walitoka nyuma kwa Bao la
Jamie Vardy na kuongoza Bao 1-0 hadi Mapumziko lakini Kipindi cha Pili Netherlands wakaigeuza Gemu.
Holland walisawazisha kwa Penati ya Vincent Janssen baada Danny Rose kuunawa Mpira na kupata Bao la ushindi kupitia Luciano Narsingh.
MAGOLI:
England 3
-Vardy, 41'
Netherlands 2
-Janssen, 50' [Penati]
-Narsingh, 77’
Mfululizo wa Mechi hizi za Kirafiki na Matayarisho ya Timu kushiriki Fainali za Kombe la Mataifa ya Ulaya, EURO 2016, yatakayochezwa huko France kuanzia Juni.
VIKOSI:
England: Forster, Walker, Smalling, Stones, Rose, Milner, Drinkwater, Vardy, Barkley, Lallana, Sturridge.
Subs: Clyne, Heaton, Walcott, Cahill, Jagielka, Henderson, Dier, Kane, Alli, Welbeck.
Holland: Zoet, Veltman, Bruma, Blind, Willems, Wijnaldum, Bazoer, Afellay, Depay, Janssen, Promes.
Subs: Vermeer, Karsdorp, van Dijk, Van Aanholt, Clasie, Narsingh, van Ginkel, Huntelaar, de Jong, Letschert, Vorm.
REFA: Antonio Miguel Mateu Lahoz (Spain)
MECHI ZA KIMATAIFA ZA KIRAFIKI
MATOKEO:
Jumanne Machi 29
1900 Estonia 0 Serbia 1
1900 Montenegro 0 Belarus 0
2000 Macedonia 0 Bulgaria 2
2030 Greece 2 Iceland 3
2100 Georgia 1 Kazakhstan 1
2100 Gibraltar 0 Latvia 5
2100 Portugal 2 Belgium 1
2145 Germany 4 Italy 1
2145 R. of Ireland 2 Slovakia 2
2200 England 1 Netherlands 2
2200 France 4 Russia 2
2200 Scotland 1 Denmark 0
No comments:
Post a Comment