Wednesday, 30 March 2016

KOMBE LA DUNIA 2018: URUGUAY YATWAA UONGOZI MAREKANI YA KUSINI, BRAZIL YAPOROMOKA HADI YA 6!




Uruguay wametwaa uongozi wa Kundi la Nchi za Kanda ya Marekani ya Kusini za kuwania kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia baada ya Jana kuifunga Peru 1-0.
Bao la ushindi la Uruguay lilifungwa Dakika ya 53 na Edinson Cavani.
Nao Argentina walishinda 2-0 walipocheza na Bolivia na Bao za Argentina zilifungwa na Gabriel Mercado, Dakika ya 20, na Penati ya Lionel Messi, Dakika ya 30.
Wakicheza Ugenini na Paraguay na bila ya Staa wao Neymar ambae yuko Kifungoni, Brazil walitoka nyuma kwa Bao 2-0 za Darino Lezcano, Dakika ya 40 na Edgar Benitez, Dakika ya 49, na kuambua Sare ya 2-2 kwa Bao za Dakika za 79 na 90 za Ricardo Oliviera na Daniel Alves.
Sare hii imewashusha Brazil hadi Nafasi ya 6.
Ecuador, ambao walikuwa wakiongoza Kundi hili, Jana walipigwa 3-1 Ugenini na Colombia na kushushwa hadi Nafasi ya Pili.
Kwenye Kundi hili, Timu 4 za juu zitafuzu moja kwa moja kwenda huko Urusi wakati ile ya 5 itaenda Mechi ya Mchujo na Timu ya Bara jingine ili Mshindi aende Fainali.
Mechi zifuatazo za Kanda hii zitachezwa Agosti 30.
KANDA YA MAREKANI YA KUSINI -CONMEBOL
MSIMAMO:
CONMEBOL-MAR30
Matokeo
Jumanne Machi 29
Colombia 3 Ecuador 1
Jumatano Machi 30 [jumanne kuamkia Jumatano]
Uruguay 1 Peru 0
Argentina 2 Bolivia 0        
Venezuela 1 Chile 4
Paraguay 2 Brazil 2 

No comments:

Post a Comment