Jana
huko Borg El Arab Stadium Mjini Alexandria, Wenyeji Egypt waliifunga
Nigeria 1-0 katika Mechi ya Kundi G la Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON
2017, na kujiweka pazuri mno kutinga Fainali huko Gabon
Matokeo hayo yamewatupa nje Nigeria kutoka Mashindano haya wakiwa
wamebakisha Mechi 1 ya Kundi G ambalo limebaki Timu 3 baada ya Juzi
Chad kujiondoa na matokeo ya Mechi zao kufutwa kwenye hesabu.
Bao la ushindi la Egypt hapo Jana lilifungwa Dakika ya 62 na Ramadhan Sobhy.
Sasa Egypt wanahitaji Sare tu katika Mechi yao ya mwisho Jijini Dar
es Salaam dhidi ya Tanzania ambayo bado inayo matumaini ya kufuzu ikuwa
itashinda vizuri Mechi zake 2 zilizobaki na kutwaa ushindi wa Kundi G
au kupita kwa Tiketi ya Mshindi wa Pili bora.
Kwa Nigeria ambao hawawezi tena kutwaa ushindi wa Kundi G
kilichobaki ni kuomba miujiza ya kufuzu kwa moja ta Tiketi 2 za Mshindi
Bora wa Pili.
Kwenye Kundi F, Morocco iliichapa 2-0 huko Marrakesh na kuwa Timu
ya kwanza kufuzu Fainali za AFCON 2017 huko Fabon huku ikiwa na Mechi 2
mkononi.
Bao za Morroco zilifungwa na Youssef El Arabi.
KUNDI G - MSIMAMO:
Egypt Mechi 3 Pointi 7
Nigeria Mechi 3 Pointi 2
Tanzania Mechi 2 Pointi 1
**Chad ilijitoa ( Matokeo ya Mechi zake yamefutwa)
AFCON 2017
MAKUNDI:
KUNDI A: Tunisia, Togo, Liberia, Djibouti
KUNDI B: Madagascar, DRC, Angola, CAR
KUNDI C: Mali, Equatorial Guinea, Benin, South Sudan
KUNDI D: Burkina Faso, Uganda, Botswana, Comoros
KUNDI E: Zambia, Congo, Kenya, Guinea Bissau
KUNDI F: Cape Verde, Morocco, Libya, Sao Tome
KUNDI G: Nigeria, Egypt, Tanzania, Chad
KUNDI H: Ghana, Mozambique, Rwanda, Mauritius
KUNDI I: Cote d’Ivoire, Sudan, Sierra Leone, Gabon
KUNDI J: Algeria, Ethiopia, Lesotho, Seychelles
KUNDI K: Senegal, Niger, Nambia, Burundi
KUNDI L: Guinea, Malawi, Zimbabwe, Swaziland
KUNDI M: Cameroon, South Africa, Gambia, Mauritania
MFUMO:
-Makundi yapo 13 ambapo 12 yana Timu 4 na moja lina Timu 3 lakini
Wenyeji Gabon, ambao wanafuzu moja kwa koja kucheza Fainali,
wamechomekwa Kundi hilo [KUNDI I] ambapo Mechi zao ni za Kirafiki tu.
-Mshindi wa kila Kundi [Washindi 13] na Timu 2 zitakazomaliza
Nafasi za Pili Bora zitatinga Fainali kuungana na Wenyeji Gabon na
kufanya Jumla ya Timu 16.
AFCON 2017
Matokeo
Jumanne Machi 29
Angola 0 Congo DR 2
Egypt 1 Nigeria 0
South Africa 0 Cameroon 0
Malawi 1 Ghana 2
Lesotho 2 Seychelles 1
Rwanda 5 Mauritius 0
Ethiopia 3 Algeria 3
Togo 0 Tunisia 0
Namibia 1 Burundi 3
Uganda 0 Burkina Faso 0
Liberia 5 Djibouti 0
Angola 0 Congo DR 2
Gambia 0 Mauritania 0
Sudan 1 Ivory Coast 1
South Africa 0 Cameroun 0
Morocco 2 Cape Verde 0
MSIMAMO WA MAKUNDI:
NCHI ZILIZOWAHI KUTWAA UBINGWA WA AFRIKA:
-Egypt-Mara 7
-Cameroon, Ghana-Mara 4
-Nigeria-Mara 3
-Congo DR-Mara 2
-Zambia, Algeria, Congo, Ethiopia, Ivory Coast, Morocco, South Africa, Sudan, Tunisia-Mara 1
No comments:
Post a Comment