Wednesday, 30 March 2016

MESSI ATAKA KUFIKISHA REKODI HII HAPA TIMU YA TAIFA


 


FOWADI wa Barcelona, Lionel Messi, mwenye Miaka 28, Jana alifikisha Rekodi yake ya Mabao kwa Nchi yake Argentina kufikia 50 baada ya kufunga kwa Penati wakati wakishinda 2-0 dhidi ya Bolivia kwenye Mechi ya Kanda ya Nchi za Marekani ya Kusini kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Urusi.
Idadi hiyo imemfanya Messi awe Bao 6 nyuma ya Fowadi wa zamani wa Fiorentina na AS Roma, Gabriel Batistuta, ambae aliipigia Argentina Mabao 56 na kuwa juu katika Ufungaji Bora wa Argentina.
Akiongea baada ya Mechi na Bolivia, Messi, alisema: “Ninafurahia Goli Namba 50 lakini muhimi ni kuwa tumeshinda!”
Messi, ambae ndie Mchezaji Bora Duniani mara 5 kwa kuzoa Ballon d'Or, ndie Mfungaji Bora katika historia ya Barcelona akiwa na Magoli 449, na Jumamosi huenda akafikisha idadi ya Mabao yake yote katika historia yake kufikia 500 ikiwa atafunga wakati Barcelona ikicheza na Mahasimu wao Real Madrid huko Nou Camp katika Mechi ya La Liga ambayo hubatizwa ‘El Clasico’.
ARGENTINA – WAFUNGAJI BORA:
Gabriel Batistuta: 56
Lionel Messi: 50
Hernan Crespo: 35
Diego Maradona: 34
Sergio Aguero: 32

No comments:

Post a Comment