Klabu
ya Yanga watakuwa wenyeji wa wana Kimanumanu African Sports, mchezo
utakaopigwa katika dimba la taifa jijini Dar es salaam, mchezo
utakaochezwa saa 10:30 kwa saa za Afrika Mashariki. Yanga wako katika
nafasi ya pili ya msimamo wa ligi wakiwa na alama 47 wakiwa wamecheza
michezo 20 nyumba ya wapinzani wao Simba walioko kileleni kwa alama 48
wakiwa wamecheza michezo 21. Kikosi hicho cha wanajangwani kimeshinda
michezo 14, na kwenda sare michezo mitano huku kikipoteza mchezo mmoja.
African sport wao wako katika nafasi ya 15 nafasi moja toka mwisho
wakiwa wamecheza michezo 21 wana alama 17.
No comments:
Post a Comment