Luke Shaw anaweza kuwa fiti kuichezea Manchester United kabla Msimu huu kumalizika baada ya kuruhusiwa kuanza tena Mazoezi Mwezi ujao ikiwa ni Miezi 7 tu baada ya kuvunjika Mguu wake wa Kulia mara mbili.
Shaw, mwenye Miaka 20, aliumia huko Amsterdam, Netherlands hapo Septemba 15 katika Mechi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI ambayo Man United walifungwa 2-1 na PSV Eindhoven kufuatia kukatwa na Beki Hector Moreno.
Ikiwa Shaw atarejea vizuri Mazoezini Mwezi Aprili basi anaweza kupata Mechi kabla Msimu huu wa 2015/16 kumalizika katikati ya Mwezi Mei.
Lakini, hali hii inamfanya kuikosa kuichezea Timu ya Taifa ya England hapo Juni itakapokuwa huko France kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Ulaya, EURO 2016.
Kukosekana kwa Luke Shaw kwenye Kikosi cha Man United Msimu huu kulimlazimisha Meneja Louis van Gaal kutumia Makinda wa Chuo cha Soka chao kina Joe Riley, Timothy Fosu-Mensah na Cameron Borthwick-Jackson kwenye Nafasi ya Fulbeki wa Kushoto ambayo pia Winga Ashley Young alichezeshwa
No comments:
Post a Comment