Monday, 7 March 2016

Sharapova afeli vipimo Australia Open

Nyota namba moja wa zamani wa mchezo wa Tenesi Maria Sharapova amethibitisha kushindwa vipimo baada ya kubainika alitumia dawa zilizopigwa marufuku michezoni katika michuano ya wazi ya Australia Mwaka huu.
Sharapova wa raia wa Urusi mwenye miaka 28 amepimwa na kubainika kutumia dawa za meldonium, ambazo amekua akitumia toka mwaka 2006.
Mcheza tenesi huyu mshindi wa Grand Slam kwa mara tano, alisema hakujua vikwazo atavyokuja kutana navyo. kwa miaka 10 nimekua nikitumia dawa zinazoitwa mildronate nikipewa na daktari wangu na familia yangu.
Katika siku chache zilizopita nimepata barua kutoka ITF (shirikisho la tenesi la kimataifa) na nikagundua kuwa dawa hizo zina jina jingine la meldonium,
"Ni muhimu sana kuelewa kwa miaka 10 dawa hizi hazikua kwenye orodha ya shirika la kudhibiti matumizi ya dawa zilizopigwa marufuku michezoni (Wada). "Lakini sheria zilibadilika mwezi January na kuzifanya dawa za meldonium kukatazwa, kitu ambacho sikufahamu, mwezi Desemba tarehe 22 nilipata barua pepe toka Wada kuhusu mabadiliko kwa dawa zilizokatazwa, ila sikufungua hiyo linki''

No comments:

Post a Comment