Umoja wa Ulaya na
viongozi wa Uturuki waliokutana mjini Brussels wameshindwa kufikia
muafaka wa suluhisho la mgogoro wa wahamiaji.
Uturuki inatuhumiwa
na Jumuiya ya Ulaya kuwa na wimbi kubwa la wahamiaji wanaovuka ,na
kuchukua msaada unaozidi euro bilioni tatu.kutokana na hali hiyo Umoja wa ulaya umeitaka Uturuki kuwachukua wahamiaji ambao hawakukidhi vigezo vya kupata hifadhi na kuongeza jitihada zaidi za kuwazuia kuvuka bahari ya Aegean kuelekea Ugiriki.
Raisi wa bunge la Ulaya ,Martin Schulz amesema suala la maombi ya uturuki kutaka kuongezewa euro bilioni tatu ili kulipia huduma za afya na shule kwa ajili ya wakimbizi wanaokaa nje ya kambi bado linajadiliwa katika mkutano huo wa nchi za umoja wa ulaya.
Hata hivyo Katibu mkuu wa NATO amesema mkutano huo ulioanza jana unafahamika wazi malengo yake katika nchi ya Uturuki na ukanda wa bahari ulioko upande wa ugiriki. Ameyasema wakati akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari,Jens Stoltenberg na Waziri Mkuu wa Uturuki Jens Stoltenberg.
No comments:
Post a Comment