Wednesday, 16 March 2016
SIMBA YAMVUA ISIHAKA KITAMBAA CHA UNAHODHA
Klabu ya Simba imemvua umakamu nahodha beki wake wa kati Hassan Isihaka kutokana na kitendo chake cha utovu wa nidhamu kwa kocha wa klabu hiyo Jackson Mayanja.
Afisa habari wa Simba Haji Manara amesema, mbali na Isihaka kuvuliwa unahodha kamati ya utendaji ya klabu hiyo imetangaza kumsimamisha mlinzi huyo wa kati kwa muda wa mwezi ujao tangu siku aliyopewa barua ya kusimamishwa kwa muda usiojulikana.
“Kamati ya utendaji ya klabu ya Simba imemsimamisha Hassan Isihaka kwa muda wa mwezi mmoja toka siku aliyopewa barua atajiunga na timu baada ya mwezi mmoja na katika kipindi hicho cha mwezi mmoja atakuwa akilipwa nusu mshahara”, amesema Haji Manara wakati wa mkutano na waandishi wa habari.
“Lakini kutokana na ukubwa wa klabu ya Simba na uzito wa kosa alilolifanya, amevuliwa unahodha, tarejea kama mchezaji wa kawaida”
Isihaka amesimamishwa kutokana na kumtolea kauli kali kocha wake Jackson Mayanja kwasababu ya kumuweka benchi katika mechi kadhaa hususan ya Simba na Yanga kisha kumpanga kwenye mchezo wa kombe la FA dhidi ya Singida United.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment