Tuesday, 15 March 2016

MAMBO 10 AMBAYO YANAWEZA KUTOKEA CHELSEA MSIMU UJAO

Radamel-falcaoHazardFabregas
Na Athumani Adam
Takribani mechi 9 zimesalia, kumalizika kwa msimu wa ligi kuu England 2015/2016. Bingwa mtetezi wa ligi hiyo Chelsea tayari wameutema ubingwa wa ligi pia hawamo kwenye kombe la FA wala ligi ya mabingwa Ulaya. Wapo katikati ya msimamo wa ligi, pia mabadiliko makubwa yanatarajiwa kufanyika kipindi cha majira ya kiangazi mwezi August kipindi cha usajili.
Makala hii inakupatia mambo kumi (10) yanayoweza kutokea ambayo bado hayajawa wazi hadi sasa.
  1. Nani kocha mpya wa Chelsea Msimu ujao
chelsea-fc
Ni swali la kwanza ambalo viongozi wa Chelsea wanajiuliza. Yupi ni bora kurithi nafasi ya Guus Hiddink kati ya Antonio Conte kocha wa sasa wa Italia au aliyekuwa kocha wa timu ya taifa ya Chile, Jorde Sampaoli. Tunatarajia kwa asilimia kubwa kuwepo kwa meneja mpya na tetesi zinasema mshindi wa ubingwa wa Serie A maarufu kama Scudetto akiwa mchezaji na kama kocha wa Juventus, Conte ana nafasi kubwa ya kuwa meneja mpya.
  1. Ipi hatma ya Guus Hiddink
Guus Hiddink
Kocha wa sasa, Guus Hiddink alijaribu kuirudisha Chelsea katika mstari baada ya kuanza msimu vibaya wakiwa na Jose Mourihno. Guus Hiddink ni rafiki mkubwa sana wa Bosi, Roman Abromovich, hivyo upo uwezekano wa Hiddink kutafutiwa nafasi nyingine ndani ya Chelsea.
  1. Naodha John Terry
Terry 4
Bado nahodha John Terry hajapewa mkataba mpya na Chelsea, zipo taarifa za yeye  kuondoka mwishoni mwa msimu huu. Terry anakabiliwa na majeraha ya mara kwa mara, amekosa mechi mbili dhidi ya PSG raundi ya 16 bora ligi ya mabingwa Ulaya. Upo uwezekano mkubwa wa yeye kuondoka Stamford bridge baada ya utumishi wa miaka 21.
  1. Michael Emenalo anabaki au kuondoka Stamford Bridge
Emelano
Huyu ni mkurugenzi wa ufundi wa the Blues. Anahusika na kufanya usajili ambao haukuwa na faida kwa Chelsea kwa kutumia pesa nyingi. Mfano akiwa mkurugenzi wa ufundi, alikubali kusajiliwa kwa Radmel Falcao akiwa majeruhi kutoka Manchester united. Baada ya kutumia takribani euro milioni 60 kusajili wachezaji 11 wasio na faida upo uwezekano wa kutokuwepo msimu ujao
  1. Muda wa Eden Hazard kuuzwa au kubaki
Eden Hazard-PSG
Eden Hazard hakuwa na mwanzo mzuri msimu wa 2015/2016 ulipoanza. Taarifa zinasema anatakiwa na PSG, je upi uwezekano wa Chelsea kukubali au kukataa ofa za PSG na Real Madrid endapo akionesha kiwango bora kwenyefainali za Euro 2016.
  1. Wachezaji gani wengine kuhama msimu wa kiangazi?
during the Barclays Premier League match between Chelsea and Newcastle United at Stamford Bridge on February 13, 2016 in London, England.
Chelsea haipo ligi ya mabingwa Ulaya msimu ujao. Upi uwezekano wa kuzuia nyota wake wengine kama Oscar, Costa na kipa Thibaut Courtois endapo zikitokea ofa nono za kuwataka.
  1. Wachezaji gani kuhamia msimu mpya
Mahrez
Zipo habari za Antonio Conte kupendekeza wachezaji kadhaa, ili kufanya nao kazi msimu ujao. Yupo kiungo Paul Pobga na kiungo wa Roma Rodja Nainggolan. Je ni rahisi kiasi gani kupatikana kwa wachezaji hawa?
  1. Kurudi nafasi za juu ligi kuu England
Chelsea-on table
Kutokuwepo Champion League japo kwa msimu mmoja, vitu viwili vinapotea kwa haraka ambavyo ni fedha na heshima ya klabu. Pia kuna uwezekano wa wachezaji nyota kuhama na kutokubali kuhamia timu yako.  Roman Abromovich kipi anataraji kwa kocha mpya, anaweza kuwarudisha nafasi za juu ligi kuu England
  1. Matumizi ya wachezaji wa Academy
Chelsea U21 d
Sera ya klabu ni kununua wachezaji kwa bei ya juu licha ya kuwepo wachezaji wengi vijana wa academy. Upo uwezekana wa baadhi ya vijana wa academy kupewa nafasi msimu ujao.
  1. Conte kuchelewa kuanza kazi
conte
Conte ambaye ni kocha wa Italia atakuwa kwenye Euro 2016. Kama atafika mbali kwenye mashindano atachelewa kujiunga na Chelsea msimu ujao.

No comments:

Post a Comment