Siku
kadhaa baada ya mwanachama wa siku nyingi wa Chama cha Mapinduzi,balozi
Juma Mwapachu, kurejea katika chama hicho baada ya kukihama wakati wa
harakati za Uchaguzi mkuu wa mwaka jana, kimekiri kuwa kuna haja ya
kusikiliza hisia za wanachama wake na kuangalia upya namna gani
wanachama wa Chama hicho walioondoka na kwenda kujiunga na vyama vingine
wanapokelewa kufutia mazingira ya siasa yalivyo sasa.
Katibu
Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana , ametoa kauli hiyo jijini Dar Es
Salaam,wakati wa mkutano na waandishi wa habari, uliolenga kumtambulisha
Mjumbe wa Halmashauri kuu Ya Taifa ya Chama hicho Christopher Ole
Sendeka, kuwa msemaji wake, kuchukua nafasi ya Nape Nauye, ambaye sasa
ni waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Bwana
Kinana, amekiri kuwa ni vyema sasa CCM ikae na kutengeneza namna ya
watu fulani kurudi ama kutorudi kabisa katika chama hicho kwa kuwa kwa
sasa utaratibu unatambua mchakato kumrejesha mwanachama bila kuangalia
alitoka kwa mtindo upi.
Katibu Mkuu huyo wa CCM, ameenda mbali zaidi na kusema kuwa lazima chama hicho kiheshimu hisia za wanachama wake.
Akizungumza
baada ya kutambulishwa, Ole Sendeka amesema CCM kinampongeza Rais John
Magufuli kwa utendaji wake na kwamba huo ndio msimamo wa Chama na
kukanusha maeneo yanayoelezwa kwamba huo ni udikteta na uonevu
No comments:
Post a Comment