Saturday, 5 March 2016

AZAM, YANGA, ZAIPA SIMBA NAFASI YA KUONGOZA VPL

Ramadhani Singano 'Messi' akimkabili vilivyo beki wa Yanga Vicent Bussou


Ramadhani Singano ‘Messi’ akimkabili vilivyo beki wa Yanga Vicent Bussou
Mchezo wa marudiano wa raundi ya pili wa ligi kuu kati ya Azam FC ambao ndiyo walikuwa wenyeji wa mchezo huo umemalizika kwa timu hizo kutoka sare ya kufungana magoli 2-2 mchezo ambao umechezwakwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
Azam walianza kufunga bao la kwanza dakika ya 12 ambalo lilitokana na kujifunga mlinzi wa Yanga Juma Abdul baada ya Kipre Tchetche kupiga shuti ambalo lilipanguliwa na golikipa wa Yanga Ally Mustafa ‘Barthez’ kisha Juma Abdul akajifunga wakati akiwa katika harakati za kuokoa.
Kikosi cha Yanga kilichoanza dhidi ya Azam FC
Kikosi cha Azam FC kilichoanza dhidi ya Yanga SC
Juma Abdul akaisawazishia Yanga bao hilo dakika ya 28 kwa shuti kali ambalo lilijaa moja kwa moja wavuni likimshinda golikipa wa Azam Aishi Manula.
Yanga wakapata bao la pili mfungaji akiwa ni Donald Ngoma aliyepasia nyavu dakika ya 42 kabla ya John Bocco kusawazisha na kuufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya bao 2-2.
Kikosi cha Yanga kilichoanza dhidi ya Azam FC
Kikosi cha Yanga kilichoanza dhidi ya Azam FC
Takwimu unazotakiwa kuzifahamu
  • Azam vs Yanga walikuwa wanacheza mechi yao ya 16 kwenye ligi (VPL). Yanga wakiwa wameshinda mechi 5 wakati Azam wakishinda mechi 5 huku timu hizo zikiwa zimetoka sare mara 5.
  • Sare ya leo (2-2) imekuwa ni sare ya sita kati ya michezo 16 ambayo timu hizo zimekutana kwenye ligi, huku ikiwa ni sare ya tano mfululizo kwenye michezo mitano ambayo timu hizo zimekutana hivi karibuni.
    Benchi la ufundi la kikosi cha Azam FC likiongozwa na kocha Stewart Hall (kushoto)
    Benchi la ufundi la kikosi cha Azam FC likiongozwa na kocha Stewart Hall (kushoto)
  • Mwaka uliopita timu hizo zilikutana mara tatu (3) mara ya kwanza ilikuwa robo fainali ya michuano ya CECAFA Kagame Cup mwezi Julai, 2015 na hadi muda wa kawaida wa mchezo unamalizika matokeo yalikuwa 0-0 Yanga wakapoteza kwa changamoto ya mikwaju ya penalti. Ngao ya Jamii mwezi Septemba, 2015 na kwa mara nyingine dakika 90 zilimalizika kwa matokeo ya 0-0, safari hii Yanga walishinda katika changamoto ya mikwaju ya penalty. Baada ya sare ya 1-1 katika VPL mwezi Disemba, 2015 timu hizo zilikutana tena Januari hii katika hatua ya makundi ya michuano ya Mapinduzi Cup huko Visiwani Zanzibar na mechi hiyo iliyokuwa na ubabe mwingi ilimalizika kwa sare ya kufungana 1-1.
    Kocha mkuu wa Yanga Hans vsn Pluijm (kulia) akiwa na benchi zima la ufundi la Yanga
    Kocha mkuu wa Yanga Hans vsn Pluijm (kulia) akiwa na benchi zima la ufundi la Yanga
  • Mwaka huu timu hizo zimekutana mara mbili, mchezo wa kwanza ulikuwa wa michuano ya Mapinduzi Cup huko Visiwani Zanzibar na mechi hiyo iliyokuwa na ubabe mwingi ilimalizika kwa sare ya kufungana 1-1.
  • Kikosi cha Yanga kilichoanza kwenye mchezo wa leo dhidi ya Azam kilikuwa na wachezaji watano wa kigeni, Vicent Bossou, Mbuyu Twite, Thaban Kamusoko, Amis Tambwe na Donald Ngoma. Azam wao waliwaanzisha wachezaji watatu wa kigeni ambao ni Pascal Wawa, Jean Baptist Mugiraneza na Kipre Tchetche.Azam vs Yanga 2
  • Timu hizo zimecheza mechi ya 20 (kila timu) huku zikifungana pointi zote zikiwa na pointi 47 lakini Yanga inaendelea kuongoza ligi kwa tofauti ya magoli dhidi ya Azam huku Simba ikiwa nafasi ya tatu na pointi zake 45.
    Donald Ngoma (kushoto) na David Mwantika (kulia) wakitunishiana misuli
    Donald Ngoma (kushoto) na David Mwantika (kulia) wakitunishiana misuli
  • Matokeo ya leo ya Azam vs Yanga yanatoa mwanya kwa Simba kupanda kileleni mwa ligi endapo itashinda mchezo wake dhidi ya Mbeya City kwasababu itakuwa imefikisha pointi 48 na kuziacha Yanga na Azam zikiwa na pointi zao 47.
    Wachezaji wa Azam na Yanga wakikumbatiana kuashiria fair play baada ya mchezo kumalizika
    Wachezaji wa Azam na Yanga wakikumbatiana kuashiria fair play baada ya mchezo kumalizika
    Didier Kavumbagu na Frank Domayo ni wachezaji wa Azam ambao walikuwa wakicheza dhidi ya timu yao ya zamani (Yanga) baada ya kuihama timu hiyo wakiwa wameitumikia kwa misimu kadhaa.

No comments:

Post a Comment