Kocha Wenger amempa lawama mchezaji wake Francis Conquelin
kwa kupata kadi nyekundu ambapo anasema alii-cost club yake. Kabla ya
kadi nyekundu hiyo Arsenal walikua wanatawala mchezo na kuongoza kwa
goli moja bila.
Arsene Wenger anasema kwamba wakati wa mapumziko walimpa
onyo mchezaji huyo kwa uchezaji wake ikiwa tayari ana kadi ya njano.
Kipindi cha pili alicheza rafu nyingine na kupewa kadi ya nyekundu.
Wenger anasema amekua dissapointed na kadi aliyopewa mchezaji wake
ambapo imepunguza nguvu ya team nzima.
Sio Wenger peke yake lakini hadi mashabiki kwenye mitandao
wameonyeshwa kuchukuia kwa kadi nyekundu ile ambayo amepewa mchezaji
huyo.
Baada ya kadi hiyo dakika ya 55, Spurs waliongoza mchezo
huo na kufunga magoli mawili ndani ya dakika 2 kabla ya Sanchez kuja
kusawazisha dakika ya 76. Hadi sasa Arsenal wana points 52 na mechi 29
wakati Leicester City wapo nafasi ya kwanza wanaongoza kwa points 57 na
michezo 28.
No comments:
Post a Comment