Mechi ambayo imeisha kwa magoli 2-2 na kuipa nafasi nzuri
Leicester City kama wakishinda mechi ya leo dhidi ya Watford imefanyika
kwenye uwanja wa White Hart Lane. Wakati mechi inaendelea ndani nje
kulikua na fujo kati ya mashabiki na polisi ambapo chanzo kamili cha
fujo hizo hakijajulikana ni nini.
Fujo hizo zilipelekea hadi mashabiki wengine kupasuka na
kuanza kutoka damu hata kabla hawajaingia ndani ya uwanja.Kutokana na
fujo hizo polisi walitumia hadi farasi kuleta utulivu eneo la tukio ili
mambo yaende kama yalivyopangwa. Mwisho wa siku mechi imeisha, mashabiki
wameumizwa lakini ndio uhalisia kwenye viwanja vingi vya michezo lazima
watatoke watu wanaotaka kuvunja amani.
No comments:
Post a Comment