Saturday, 9 January 2016

YAYA TOURE : MIMI NILISTAHILI KUPATA ILE TUZO YA CAF WALICHOKIFANYA NI AIBU

yaya0
Akiwa mwenye jazba, Yaya Toure amekuja juu na kuponda kunyimwa kwake Tuzo ya 5 mfululizo ya Mchezaji Bora wa Afrika kwa Mwaka 2015 na kuitwa uteuzi uliofanyika Juzi huko Abuja, Nigeria kuwa ni ‘uchafu’ na umiletea ‘aibu’ Bara la Afrika.
Toure, Kiungo wa Manchester City na Timu ya Taifa ya Ivory Coast, alibwagwa kwa Kura 7 tu na Straika wa Gabon na Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang.
Toure anaamini yeye ndie alistahili kuizoa Tuzo hiyo baada ya kuiongoza kama Nahodha Nchi yake Ivory Coast kutwaa AFCON 2015, Kombe la Mataifa ya Afrika mapema Mwaka Jana.
Akiongea na Radio France International hapo Jana, Toure alieleza: “Nadhani hii inaifanya iwe aibu ya Afrika!”
Aubameyang, akiwa Mchezaji wa kwanza toka Gabon kutwaa Tuzo ya Mchezaji Bora Afrika, amefunga Bao 29 kwenye Bundesliga katika Mwaka 2015 zikiwamo Bao 18 Msimu huu na pia kufunga Bao 7 kwenye EUROPA LIGI.
Lakini kwenye AFCON 2015, Gabon ilitolewa Raundi ya Kwanza tu kwenye Mashindano hayo yaliyochezwa Nchini Equatorial Guinea.
Akifafanua kuchukizwa kwake, Toure alieleza: "Waafrika hawaeleza umuhimu wa Afrika kwetu! Tunatoa umuhimu kwa yale yanayotokea mahali kwingine kupita Barani kwetu. Hii inaumiza. Yaya atajitunza mwenyewe na kuiacha Afrika ijitazame yenyewe. Kama ninavyoambiwa mara nyingi, ‘usiijali sana Afrika kwani Afrika itakuwa ya kwanza kukumwaga!’".
Tuzo ya Mchezaji Bora Afrika kwa Mwaka 2015 kwa wale wachezao ndani imezolewa na Supastraika wa Tanzania, Mbwana Samatta, anaechezea Klabu ya TP Mazembe ya huko Lubumbashi, Congo DR.

No comments:

Post a Comment