Wednesday, 6 January 2016

UNATAKA KUOA AU KUOLEWA MWENZIO AWE NA SIFA HIZI HAPA...............

Image result for MAPENZI YA FURAHA
1.Anakupigia simu mara kwa mara kukujulia hali:
Anakupigia simu asubuhi kukujulia hali kama umeamkaje, mchanaatakupigia simu kujua umeshindaje na kama umeshakula chakula cha mchana, midamida ya kati kati ataku check kwa message kujua kama uko sawa na usiku atakupigiasimu na kupeana stori mbili tatu kisha atakutakia usimu mwema.

2.Hataki mkutane kimwili kabla ya ndoa nahuenda akawa hajawahi kuwa na uhusiano na mwanamke tangu azaliwe:
Mwanaume mwenye sifa hii mara nyingi hutawaliwana aibu, swala la kukutana kimwili halipo katika mawazo yake hata kama muwewawili tu mmejifungia chumbani wala hanamihemko ya ngono, kwake yeye ni kupiga soga na kisha anaondoka zake kurudikwake. Ndoto yake ni kusubiri hadi mfunge ndoa.

3.Ana mazoea ya kukununulia zawadi au kukupa fedha za matumizi mara kwa mara:
Hivi ndivyo wasichana wengi wanavyopendawatendewe na wapenzi wao, kununuliwa zawadi, kupewa fedha za matumizi nakununuliwa muda wa maongezi kwenye simu, yaani kila akikutana na mpenzi wakeanamwaga pesa, yaani ni pesa pesa pesa hata huwazi kuhusu chochote maana mwanaume yupo kuhakikisha unapata kilakitu. Huyu ndiye husband material haswa.

4 Hanywi pombe wala havuti sigara:
Mwanaume wa aina hii huwavutia wasichana wengi, yaani hajui ladha ya pombe walasigara. Jamani tuacheni utani mwanaume anayekunywa pombe na kuvuta sigara hanamvuto maana hata kiss unajishauri kwa jinsi harufu ya kinywa isivyo rafiki wakupigana kiss, unaweza hata kutapika.

5.Siyo mtu wa kwenda Klabu wala kujirusha kwenye matamasha ya usiku (Party):
Mwanaume hatulii kila siku analala usikuwa manane kwa sababu ya kupenda kujirusha, inawezekana hanywi pombe wala havutisigara, lakini kwa kujirusha ndiyo hobby yake huyu hafai,ukimpata mwanaumeambaye kila akitoka kazini ni nyumbani na hata kama ni kutoka anakuwa anakwendakutembelea marafiki zake waliooa au ndugu zake na kurudi nyumbani mapema, yaanikampani yake ni watu wazima wenye kuwajibika sawa sawa kwa familia. Huyu nimwanaume wa kufaa kuolewa naye

6.Awe anakumbuka Birthday yako:
Yaani mtu wa kwanza kukuamsha alfajiri na kukuambia Happy Birthday anakuwa niyeye na baadaye anakushangaza na zawadi na sherehe ndogo inayowajumuishamarafiki zako. Yaani hasahau siku yako ya kuzaliwa, na kila mwaka anabadilishanamna ya kukushangaza tarehe ya siku yako ya kuzaliwa ikifika. Jambo hilihuwapa raha sana wasichana wa siku hizi.

7.Ni mtu mwenye hofu ya Mungu:
Kama ni Mkristo yaani yeye na kanisa kanisa na yeye na anashiriki kwenye kamatimbalimbali za kanisa na anakuwa na majukumu makubwa katika kanisa na kama niMuislamu hivyo hivyo, anakuwa mtu wa hamsa swallati na mshiriki mkubwa katikashughuli za msikitini kwa kujitolea

8.Unaweza kukisia wakati wowote kwamba yuko wapi na anafanya nini na ukawa hujakosea: Anaweza akawanyumbani, kazini, kanisani akihudhuria masomo ya biblia au msikitini akijisomeaQuran au yuko kwa rafiki yake au ndugu yake waliyeshibana na ukawa hujakosea.

9.Anapenda sana kusoma:
Mwanaume mwenye kupenda kujisomea vitabu mbalimbali vya maarifa na kufuatiliahabari mbalimbali kuhusu kinachoendelea duniani kuanzia mtandaoni hadi kwenye TV, yaaniukifika kwake unakutana na Big flat screen na bookshelf kubwa limeshehenivitabu vya maarifa ya kila aina.Mwanaume wa aina hii atakuwa na uelewa mpanasana na utambuzi wa hali ya juu, huyu atakuwa ni mtu wa kuyachukulia mambo kwaumakini wa hali ya juu na hadhari kubwa, ni mtu wa kufanya maamuzi bila kukurupuka,huyu naye ni husband material.

10.Mpole na mnyenyekevu:
Yaani unakutana na mwanaume mpole namnyenyekevu hadi raha, akiongea anakuwa kama vile hataki, lakini kuna wakatianakuwa na masihara na utani unaokufanya ujisikie furaha kuwa naye wakati wote.Masihara na utani wake unakuwa umebeba ujumbe wenye hekima na busara kiasikwamba kila unapokuwa naye unajikuta umejifunza kitu kipya.

11.Mpenda watoto: Hii sifa ilitakiwa iwe ni namba moja sema tu nimeghafilika, kwakweli mwanaume hawezi kuwa na sifa za kuitwa husbanda material kama amekosa hiisifa ya kupenda watoto na familia yake. Mwanaume husband materiala anatakiwaawe anajua kubadilisha mtoto nepi, kumlisha mtoto, kubembeleza mtoto akiliausiku wakati mama akiwa amelala kwa uchovu na pia awe anajua kuchagua zawadimbalimbali wanazopenda watoto, au awe na ratiba ya kuwatoa watoto kwenye mitokoyenye kuwavutia watoto kutokana na uwepowa michezo mbalimbali inayowafurahisha watoto.

12. Mwanaume anayeweza kumuua nyoka akafa:
Hapa simaanishi nyoka wa mdimu,namaanisha mwanaume asiyeweka visasi, mkitofautiana mnazungumza na kuyamaliza na kusahau. Huyu ni mwanaume mwenye sifa za kuitwa husband material.Kama ikitokea mwanaume ana sifa zote hizo nilizozitaja hapo juu au angalau nusuyake basi huyo anastahili kuitwa husband material.

No comments:

Post a Comment