Thursday, 7 January 2016

Mwenyekiti Chadema apongeza kasi ya JPM

MWENYEKITI wa Chadema mkoa wa Rukwa, Zeno Nkoswe amepongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kutumbua majipu na vijipu. Akizungumza katika mahojiano na gazeti hili, Nkoswe alisema ni jambo ambalo ni jema kwa serikali inayoongozwa na Rais John Magufuli kuonesha mapema kwamba haina utani dhidi ya vitendo vya rushwa, ufisadi na ubadhirifu wa fedha za umma. Nkoswe ambaye aliwahi kuwa Mwenyekiti wa kwanza wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Rukwa kwa miongo miwili; 1977 hadi 1987 alijiunga Chadema mwaka 2010 baada ya kuvuliwa uanachama wa CCM.
“Binafsi nimefurahishwa sana na hatua za serikali hii kwa sababu uozo ambao tumekuwa tukiupigia kelele, si viongozi wa upinzani bali pia wananchi wa kawaida, ni haya ambayo sasa tunayaona na kuyasikia,” alisema Nkoswe.
Aliongeza: “Kazi hii anayoifanya Rais ni ngumu na nzito na kama anavyosema mwenyewe Rais, tumwombee. Tumwombee kwani endapo atafanikiwa katika hili, nchi yetu, mbali na kuwa na maendeleo lakini pia itakuwa ya heshima duniani.”
Alisema ameguswa na kitendo cha makatibu wakuu na manaibu wao kula kiapo cha maadili hadharani akisisitiza kuwa kiapo hicho ni sawa na Azimio la Arusha, lingine lililosifika kwa kusimamia madhubuti maadili ya uongozi.
“Hatua hii ya Rais wetu Magufuli kupambana na kuanika uozo wote naweza kumfananisha na Hayati Edward Sokoine. Pia zinafanana na hatua za mwanzo alizochukua Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere dhidi ya viongozi waliokuwa wakijilimbikizia mali na kuwakoga wananchi mara tu baada ya Uhuru,” alisema.
Hata hivyo, aliitaka serikali kuwaanika hadharani waliohusika na kashfa za Richmond, Meremeta, rada, EPA na zote zilizojiri huko nyuma. Alihimiza Watanzania k

No comments:

Post a Comment