Kutokana
na matukio ya kiuhalifu yanayoendelea katika baadhi ya maeneo nchini,
leo August 25 2016 Jeshi la Polisi limepiga marufuku mikutano yote ya
kivyama ndani na nje ili kuzuia machafuko ya amani yanayoendelea
kujitokeza katika kipindi hiki.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam Kamishna wa Polisi CP Nsato Marijani amesema…>>>’Jeshi
la polisi halikuzuia mikutano ya ndani ya siasa kwasababu tulikuwa
tunaamini ni mikutano iliyokuwa ikizungumzia maendeleo ya wananchi‘
‘Lakini
sasa tumebaini kwamba mikutano hiyo imekuwa ikitumika kucchochea
wananchi na kuwahamasisha kuvunja sheria za nchi na kufanya mapambano na
jeshi la polisi‘ –CP Nsato Marijani
‘Kwasababu
hiyo basi kwa hali ya kutumia mikutano ya ndani kuchochea watu kuvunja
sheria na kupambana na askari, hivyo basi kuanzia sasa jeshi la polisi
nchini linapiga marufuku mikutano yote ya ndani‘ –CP Nsato Marijani
No comments:
Post a Comment