Bw Cameron ambaye ameongoza kampeini ya Uingereza kusalia katika muungano wa umoja wa ulaya (EU) amesema uamuzi wa raia wa taifa hilo kubwa dunaini kujitoa kwenye umoja wa ulaya umempa mshutuko mkubwa ikiwa ni pamoja na watu mashuhuri duniani.
Akitoa tamko hilo mbele ya waandishi wa habari nje ya afisi yake jijini London, Bwana Cameron amedai kuwa anahisi yeye sio mtu muhimu wa kuliongoza taifa hilo kwa ufanisi chini ya uamuzi kama uliofikiwa na raia wanaopendekeza Uingereza kujitoa kwenye umoja wa ulaya.
Kwa upande wa waliokua wakiongoza kampeni kwa taifa hilo kujitoa,wameonekana kusheherekea matokeo hayo.
No comments:
Post a Comment