Thursday, 2 June 2016

VIDEO: TUKIO HILI LA RONALDO KWA GRIEZMANN NI JIBU TOSHA KWA WABAYA WAKE

Ronaldo-Griezman

Cristiano Ronaldo aliibuka shujaa wa Real Madrid kwenye fainali ya Champions League dhidi ya Atletico Madrid baada kufunga penati muhimu iliyowapa ubingwa Real.
Kwa upande mwingine lilikuwa ni pigo kubwa kwa Atletico baada ya kushuhudia wakikosi tena ubingwa huo ndani ya miaka miwili ambayo wamekutana na timu hiyo hiyo.
Antoine Griezmann, kama ilivyo kwa upande wa Juanfran, alijiikia vibaya sana baada ya mchezo huo. Mfaransa huyo alikosa penati katika kipindi cha pili cha mchezo, penati ambayo pengine ingewahakikishia Attletico ushindi kutokana na baadaye kupata goli dakika ya 79 ambalo sasa lilikuwa ndilo la kusawazisha.
Baada ya mchezo kumalizika, Griezmann alikuwa ni mwenye huzuni kubwa isiyobebeka, lakini shukrani za dhati ziende kwa Cristiano Ronaldo ambaye alitumia muda wake mfupi uwanjani kumfariji walau asiwe na mawazo yaliyopitiliza.
Ronaldo amekuwa akishutumiwa kuwa na majivuno lakini kadri siku zinvyosonga mbele amekuwa ‘akiwa-prove wrong’ wabaya wake.
Angalia video hapa chini Ronaldo alivyompoza Griezmann baada ya timu ya Atletico kushindwa kutwaa taji la Champions League.
 
 

No comments:

Post a Comment