Sunday, 29 May 2016

Walinda amani watano wauawa nchini Mali


Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Mali umesema kuwa walinda amani wake watano wameuawa na wengine wamejeruhiwa vibaya katika shambulizi lililotokea katikati ya mji wa Mopti. Waathirika wanatokea nchini Togo.Gari lao lilipatwa na moto kabla ya kukanyaga bomu la ardhini,na kisha kulipuka.Waziri wa masuala ya kigeni nchini Mali, Abdoulaye Diop, ametuma salam za rambirambi katika mitandao ya kijamii kwa UN na nchi ya Togo.Vifo vyao vimekuja wakati dunia ikiadhimisha siku yawalinda amani.Mwaka uliopita walinda amani 129 kutoka umoja wa mataifa walipoteza maisha katika nchi 16 wanazofanyia shughuli zao.

No comments:

Post a Comment