Olivier Giroud aliripotiwa kuzomewa na mashabiki wa Ufaransa kabla ya mchezo wao dhidi ya Cameroon uliopigwa leo. Wakati akipanda basi la timu, mashabiki walikuwa wakipiga kelele na kusema kwamba Karim Benzema ndiye anapaswa kwenda michuano ya EURO na sio yeye.
Licha ya figisu hizo kutoka kwa mashabiki hao, mshambulizi huyo wa Arsenal amewafunga midomo mashabiki hao baada ya kufunga goli maridhawa baada ya kupata pasi murua kutoka kwa nyota wa Juventus Paul Pogba.
Pogba alitoa pasi hiyo kutoka upande wa kushoto baada ya kuwahadaa mabeki wa Cameroon na Giroud kupiga shuti kali aina ya volley na kutinga wavuni.
Katika mchezo huo, Ufaransa wameshinda mabao 3-2, magoli mengine ya Ufaransa yamefungwa na Blaise Matuidi (dakika ya 20) na Dimitri Payet (dakika ya 90) huku magoli ya Cameroon yakifungwa na Vincent Aboubakar (dakika ya 22) na Eric Maxim Choupo-Moting (dakika ya 88).
No comments:
Post a Comment