Sheria mpya kali dhidi ya uvutaji na mauzo ya bidhaa za tumbaku zimeanza kutekelezwa nchini Uganda.
Watu
wanaovuta sigara wakiwa maeneo ya burudani na migahawa sasa watapigwa
faini ya dola 60 au kifungo cha hadi miezi miwili jela.Pia wavutaji sigara watahitajika kuwa umbali wa takriban mita 50 kutoka maeneo ya umma kama vile shule na hospitali.
Serikali pia imepiga marufuku kuuzwa kwa sigara moja na kudhibiti zaidi matangazo ya sigara na kuzwa kwa bidhaa za tumbaku kwa watu walio chini ya umri wa miaka 21.
No comments:
Post a Comment