Mara baada ya msimu wa ligi kuu ya Uingereza kumalizika kiungo mchezeshaji Mesut Ozil anekipiga na klabu ya Arsenal ametumia muda wake wa mapumziko huku akijiandaa kwenda kuipeperusha bendera ya Ujerumani kwenye michuano ya Euro,kwa kutembelea kambi ya wakimbizi nchini Jordan na kucheza mpira na watoto kwenye kambi hiyo.
Kiungo huyo aliyeshinda kombe la dunia mwaka 2014 ametembelea kambi hiyo ya wakimbizi wanaotoka kwenye za mashariki ya kati hasa zile zenye mashafuko ya kisiasa na kuelezewa kwa ufupi hali ya maisha ya watoto ilivyokuwa ngumu katika kambi hiyo huku akilakiwa na watoto walifurahishwa na kitendo cha Star huyo kuwatembelea mbapo Ozil aligawa mipira ya soka, cap za baseball baada ya kucheza pamoja na watoto hao.
Mashabiki wa Arsenal huenda wakahuzunishwa kutokana na kitendo cha Ozil kuamua kusogeza mbele mazungumzo ya kuongeza mkata mpya na klabu hiyo hadi pale fainali za mataifa ya Ulaya zitakapomalizika nchini Ufaransa.
“Bado nina miaka miwili kwenye mkataba wangu na Arsenal na kwasasa naweka akili yangu yote kwenye michuano ya Euro 2016, kitakachotokea kuhusu Arsenal tutaona baadaye sote kwa pamoja”Ozil aliwajibu waandishi wlipotaka kujua mstakabali wake na Arsenal.
Ozil amefanikiwa kupiga pasi nyingi za magoli kwa upande wa Arsenal msimu huu kwa kufanikiwa kutengeneza magoli 19 kwenye Premier League.
No comments:
Post a Comment