Thursday, 19 May 2016

'Maria Sharapova huenda asicheze tena'


Aliyekuwa mchezaji nambari moja wa tenisi kwa upande wa wanawake Maria Sharapova huenda asicheze tena baada ya kubainika kwamba amekuwa akitumia dawa za kusisimua misuli, rais wa shirikisho la mchezo wa tenisi nchini Urusi amesema.
Raia huyo wa Urusi mwenye umri wa miaka 29 alipatikana na dawa ya Meldonium katika michano ya Australia Open mnamo mwezi Januari.
Alipoulizwa iwapo Sharapova atashiriki katika michuano mengine,Shamil Tarpishchev aliambia kitengo cha habari cha R-Sport kwamba hadhani, akiongezea kwamba mshindi huyo mara tano wa Grand Slam alikuwa katika hali mbaya.
Mnamo mwezi Machi,Sharapova alisema kuwa alikuwa tayari kuendelea na tenisi.
Shirikisho la kimataifa la mchezo wa tenisi ITF lilimpiga marufuku kwa mda Sharapova mnamo tarehe 12 mwezi Machi.
Anasubiri kusikia adhabu yake kamili ,ambayo huenda ikawa marufuku ya miaka minne,ijapokuwa wataalam wanasema huenda akapewa marufuku ya miezi sita au 12.

No comments:

Post a Comment