Klabu ya soka ya
Aston villa ambayo imeteremka daraja msimu huu katika ligi kuu ya
England,hatimaye imenunuliwa na tajiri wa kichina Tony Xia ambaye ni
mfanya biashara aliyewekeza katika sekta ya Michezo,Utalii,kilimo na
afya.
Xia ameinunua Aston Villa kwa gharama ya dola milioni tisini
(90), amesema amekuwa ni shabiki mkubwa wa klabu hiyo kwa miaka mingi
ingawaje hajafurahishwa na matokeo mabovu ya msimu huu amabayo
yamepelekea timu hiyo kushuka daraja.Aston villa imeshuka daraja baada ya kuwa timu ya mwisho katika msimamo nafasi ya ishirini ikiwa na alama kumi na saba .
No comments:
Post a Comment