ameshasaini Mkataba wa kuwa Meneja mpya wa Manchester United. Man United itamtangaza rasmi Ijumaa baada kuliarifu rasmi Soko la Hisa la New York ambako imesajiliwa kama Kanuni za Makampuni yaliyosajiliwa huko yanavyopasa kufanya.
Mazungumzo kati ya upande wa Mourinho ukiongozwa na Wakala wake Jorge Mendes na Makamu Mwenyekiti Mtendaji wa Man United Ed Woodward yalichukua Siku 3 Jijini London na kukamilika Leo kwenye Saa 11 Jioni kwa majira ya London ambayo ni Saa 1 Usiku kwa Saa za Tanzania.
Mourinho amekuwa hana kibarua tangu Desemba alipoondoka Chelsea na anambadili Louis van Gaal alietimuliwa Jumatatu iliyopita ikiwa ni Siku mbili tu baada ya kuiongoza Man United kutwaa FA CUP kwa kuichapa Crystal Palace 2-1 Uwanjani Wembley Jijini London.
Inatarajiwa Mourinho atatua Old Trafford akiwa na Msaidizi wake wa muda mrefu Rui Faria ambae amekuwa nae kila anapokwenda kuanzia huko FC Porto, Chelsea, Inter Milan na Real Madrid.
Lakini pia zipo habari kwamba Meneja Msaidizi wa Man United Ryan Giggs atabakia Old Trafford na Mourinho mwenyewe ameridhia kuwa nae.
MOURINHO – WASIFU:
Jina kamili: José Mário dos Santos Mourinho Félix
Tarehe ya Kuzaliwa: 26 Januari 1963 (Miaka 53)
Mahali pa kuzaliwa: Setúbal, Portugal
Klabu alizoongoza kama Meneja:
-2000 Benfica
-2001–2002 União de Leiria
-2002–2004 FC Porto
-2004–2007 Chelsea
-2008–2010 Inter Milan
-2010–2013 Real Madrid
-2013–2015 Chelsea
Mataji aliyotwaa:
FC Porto
-Primeira Liga: 2002–03, 2003–04
-Taça de Portugal: 2002–03
-Supertaça Cândido de Oliveira: 2003
-UEFA Champions League: 2003–04
-UEFA Cup: 2002–03
Chelsea
-Premier League: 2004–05, 2005–06, 2014–15
-FA Cup: 2006–07
-Football League Cup: 2004–05, 2006–07, 2014–15
-FA Community Shield: 2005
Inter Milan
-Serie A: 2008–09, 2009–10
-Coppa Italia: 2009–10
-Supercoppa Italiana: 2008
-UEFA Champions League: 2009–10
Real Madrid
-La Liga: 2011–12
-Copa del Rey: 2010–11
-Supercopa de España: 2012
No comments:
Post a Comment