Thursday, 26 May 2016

HAKUNA UBISHI TENA, MOURINHO KOCHA MPYA MANCHESTER UNITED

Mourinho scarf


Kwa mujibu wa matandao wa Sky Sports, Jose Mourinho ametangazwa kuwa kocha mpya wa Manchester United.
Tayari ameshasaini mkataba na tayari umeshatumwa kwenda Manchester na vuguvugu la tetesi za kocha huyo kujiunga na United zimekwisha.
Kulikuwa na ukimya baada ya Manchester United kutwaa ndoo ya FA Cup kwa ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Crystal Palace, tuliarifiwa kwamba, Louis van Gaal atatimuliwa siku ya Jumatatu na siku ya Jumanne Mourinho kupewa mikoba ya kuwa manager mpya wa Old Trafford.
Kutimuliwa kwa Louis van Gaal ndani ya Manchester United kulitangazwa usiku wa Jumatatu huku kutangazwa kwa Jose Mourinho kukichukua siku kadhaa mbele tofauti na ilivyotarajiwa.
Siku nzima ya jana ilitawaliwa na taarifa za Mourinho kujiunga na Manchester United lakini kumekuwepo na taarifa nyingine kuhusu haki za picha ya sura ya kocha huyo (image rights)
Jumatano usiku, kituo kimoja cha radio cha nchini Hispania kilithibitisha kwamba, dili la Mourinho limekamilika na wakala wa kocha huyo Jorge Mendes leo atakuwa akimalizia makubaliano ya pande mbili.
Kabla ya kukutana na maafisa wa Manchester United siku ya Jumatano, Mendes alikuwa London akishughulikia mambo ya haki miliki ya picha ya sura ya Mourinho ambapo tayari sakata hilo limeshakamilika.
Hii ndiyo taarifa rasmi kwa mujibu wa kituo cha Sky Sport-BREAKING: Jose Mourinho is appointed as the new Manchester United manager #SSNHQ https://t.co/V1BdzRmgvB
— Sky Sports News HQ (@SkySportsNewsHQ) May 26, 2016

No comments:

Post a Comment