UEFA CHAMPIONZ LIGI
Fainali
Stadio San Siro – Milan, Italy
Jumamosi Mei 28
**Saa 3 Dakika 45 Usiku
Atletico Madrid v Real Madrid
JUMAMOSI Usiku huko Italy, ndani ya Uwanja maarufu wa San Siro Jijini Milan, Klabu za Jijini Madrid, Spain ambazo ni Mahasimu, Atlètico Madrid na Real Madrid, zitapambana kwenye Fainali ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Hii itakuwa ni kama marudio ya Fainali ya UCL ya Mwaka ambayo Real walishinda 4-1 katika Dakika za Nyongeza 30 baada ya kusawazisha Bao Bao na kupata Sare ya 1-1 katika Dakika za Majeruhi za Dakika 90 za kawaida.
Njia ya kuingia Fainali: Real Madrid
Licha ya kuwekwa Kundi A na Timu ngumu Paris Saint-Germain, Real Madrid waliibuka Washindi wa Kundi hilo kirahisi baada ya kushinda Mechi 5 na Sare 1.
Kwenye Raundi ya Mtoano ya Timu 16, Real waliibwaga AS Roma kwa Jumla ya Mabao 4-0 kwa Mechi 2 na Raundi iliyofuata, Real waliteleza na kupigwa 2-0 katika Mechi ya Kwanza na Wolfsburg.
Lakini kwenye Mechi ya Pili, Nyota wao Cristiano Ronaldo aliibuka Shujaa na kupiga Bao 3 zilizowatupa nje Wolfsburg 3-0 na Real kutinga Nusu Fainali ambapo walitoka 0-0 na Man City huko Etihad huku Real wakimkosa Majeruhi Ronaldo na kisha kuwapiga City 1-0 huko Santiago Bernabeu kwa Bao la Gareth Bale.
Njia ya kuingia Fainali: Atlètico Madrid
Atlètico Madrid walisonga Mashindano haya kwa kusuasua ingawa walimaliza Washindi wa Kundi lao.
Kwenye Raundi ya Mtoano ya Timu 16 Atletico walibanwa na PSV Eindhoven na hatimae kupenya kwa Mikwaju ya Penati 8-7.
Kisha wakawavaa Mabingwa Watetezi FC Barcelona ambao waliifunga Atletico 2-1 katika Mechi ya Kwanza huko Nou Camp lakini kwenye Marudiano huko Vicente Calderon, Atletico walishinda Bao 3 na kusonga huku Staa wao Antoine Griezmann akipiga Bao 2.
Kwenye Nusu Fainali, Atletico walivaa Bayern Munich na kushinda 1-0 katika Mechi ya Kwanza huko Spain na kufungwa 2-1 huko Germany na kusonga tu kwa trufu ya Bao la Ugenini.
Mtazamo
Hii ni gemu ambayo upande wowote unaweza kushinda lakini ukichukulia kwa uzoefu, Real wako mbele kwa vile wana Mataji 10 ya Ulaya baada ya kutinga Fainali mara 14 wakati Atletico hawajawahi kutwaa Taji hili baada ya kufika Fainali mara 2 tu na kufungwa zote.
Pia Real wanae Cristiano Ronaldo ambae ndie Mfungaji Bora wa Mashindano haya Msimu huu akiwa na Bao 16 na anahitaji Bao 2 tu kuvunja Rekodi ya Kihistoria ya Bao nyingi katika Msimu mmoja wa UCL ya Bao 17 ambayo aliiweka yeye mwenyewe Msimu wa 2013/14.
Tegenezi kubwa la Atletico ni Mfaransa Antoine Griezmann mwenye Bao 7 Msimu huu kwenye Mashindano haya.
Nguvu kubwa ya Atletico ni Difensi yao ngumu lakini itapata shida sana kuwahimili Ronaldo, Bale na Benzema ambao watakuwa wakilishwa na Viungo mahiri Luka Modric na Toni Kroos.
Makocha
Real wapo chini ya Lejendari wa France Zinedine Zidane, alietwaa UCL Mwaka 2002 akiwa na Real Madrid in 2002, nah ii ndio kazi yake ya kwanza kama Kocha wa Timu kubwa baada ya kumrithi Rafa Benitez aliefukuzwa Mwezi Desemba.
Atletico wako chini ya Muargentina Diego Simeone ambae enzi zake alikuwa Kiungo Mkabaji wa Shokan a ambae ameiongoza Atletico kuanzia 2012 na kuijenga Timu hii kuwa ya Wachezaji wenye nguvu-kazi kubwa Uwanjani.
VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
REAL MADRID:
Navas; Marcelo, Ramos, Pepe, Carvajal; Casemiro, Kroos, Modric; Bale, Ronaldo, Benzema
ATLETICO MADRID:
Oblak; Juanfran, Godin, Gimenez, Filipe Luis; Saul, Gabi, Fernandez, Koke; Torres, Griezmann
REFA: Mark Clattenburg [England]
No comments:
Post a Comment