Usiku wa May 18 2016 ndio siku ambayo klabu ya Liverpool ilicheza mchezo wa fainali ya Kombe la UEFA EUROPA League dhidi ya klabu ya Sevilla kutoka Hispania, mchezo wa fainali ya Europa League ulichezwa katika uwanja wa St Jakob Park ambapo rekodi zinaonesha Liverpool hajawahi kushinda katika uwanja huo.
Mchezo huo kati ya Sevilla dhidi ya Liverpool ulianza kwa matumaini kama Liverpool wataibuka na ushindi, hiyo inatokana na Daniel Sturridge kupachika goli la mapema dakika ya 35, furaha ya Liverpool ilianza kupotea dakika ya 46 baada ya Kevin Gameiro kusawzisha goli, Coke alimaliza furaha ya Liverpool baada ya kuongeza magoli mengine mawili dakika ya 64 na 70.
Hadi dakika 90 zinamalizika Sevilla 3-1 Liverpool, licha ya Liverpool kumiliki mpira kwa asilimia 54 na Sevilla asilimia 46, walishindwa kusawazisha na kukubali kuendelea na rekodi yao ya kutopata matokeo mazuri katika uwanja wa St Jakob Park.
No comments:
Post a Comment