Thursday, 26 May 2016

Chid Benz ataroka “Sober House”baada ya kukaa kwa siku 28.

kala na chid bagamoyo


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na  meneja wa kituo hicho kilichopo Bagamoyo Tumaini Majura,alidai kuwa rapper huyo alikaa siku 28 lakini alitakiwa kukaa kwa muda wa angalau miezi mitatu ili kurudi katika hali yake ya kawaida ila kwa uamuzi wake binafsi aliamua kuondoka kituoni hapo mara baada ya meneja wa kundi la TipTop (Babu Tale) kufika kituoni hapo kumjulia hali ambapo  aling’ang’ania kuondoka naye licha ya Bau Tale na watu wengine kumsihi abaki.
Chid Benz (L) alipotembelewa kituoni hapo na Host wa kipindi cha “Harakati” cha Clouds Tv,Kalama Masood maarufu kama Kalapina.




Aidha Majura alipoulizwa maisha ya rapper huyo kituoni hapo alijibu “Kwa viongozi hayakuwa mabaya sana japo alikuwa mzito kushiriki kwenye ishu za usafi na vitu vingine,muda mwingi alipenda kupumzika na kuandika mistari lakini kuna kipindi alikuwa akijaribu kuhamasisha wenzake wagomee kitu fulani ila sisi tulikuwa tunamchukulia kama mtu wa kawaida aliyekuwa anahitaji msaada “alisema Mejura.
babu tale na chid benz                                                     Babu Tale na Chid Benz.
Hata hivyo juhudi za kumtafuta Chid Benzi na Babu Tale ziligonga mwamba kwani wote kwa pamoja simu zao zimekua zikiita bila kupokelewa.
Credit : Global Publisher.

No comments:

Post a Comment