R&B hit maker Chris Brown ameshinda
kesi ya malezi ya mtoto wake Royality dhidi ya mama wa mtoto huyo Nia
Guzman ambae kupitia mwanasheria wake alifungua mashtaka dhidi ya Brezy
akipinga Mwanamuziki huyo kumlea binti yao Royality kwa madai kuwa Chris
Brown amekua akitumia madawa ya kulevya (Bangi) na kujihusisha vurugu
mara kwa mara huku akidai kuongezewa malipo ya malezi ya binti yake
(child support allowance) kutoka $2,500 hadi $16,000 kwa mwezi.
Hata
hivyo mahakama ilimpa ushindi Chris Brown ambae kwa mujibu wa hukumu
hiyo atakua na siku 12 za kukaa na binti yake kila mwezi bila kuingiliwa
huku yeye pamoja na Mama wa binti huyo Nia Guzman wakiwa na haki sawa
juu ya malezi ya binti huyo mwenye umri wa mwaka mmoja.
Inadaiwa
kuwa ushindi wa Chris Brown dhidi ya mama watoto wake ulisababishwa na
wanasheria wa Nia Guzman kutokua na ushaihidi wa kutosha juu ya mashtaka
ya mteja wao dhidi ya Chris Brown ambae album yake mpya iliyotoka mwaka
2015 aliamua kuipa jina la binti yake “ROYALITY” kama njia njia ya
kuonesha mapenzi na mwanae.
No comments:
Post a Comment