Wachezaji wa klabu ya Azam FC, wamefanya mazoezi kwenye uwanja wa
mazoezi wa Azam Complex asubuhi ya leo, mara baada ya kuilaza Tanzania
Prisons kwa mabao 3-1 jana jioni na kutinga hatua ya nusu fainali ya
michuano ya kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup).
Baadhi ya wachezaji waliocheza dakika nyingi kwenye mchezo wa jana
leo walifanya mazoezi mepesi chini ya uangalizi wa kocha Mario Marinica,
huku wakimalizia na programu ya kurudisha mwili katika hali ya kawaida
kwa kuingia ndani ya mapipa ya maji yenye mabarafu.
Azam FC imeendelea na mazoezi hayo katika kujiweka sawa kwa mchezo
ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) dhidi ya Toto Africans,
utaofanyika Jumapili ijayo (Aprili 3) kwenye uwanja wa CCM Kirumba,
Mwanza.
Chanzo: Official Facebook Page for AzamFC
No comments:
Post a Comment