Monday, 21 March 2016

Upinzani washinda urais Benin

Rais mteule wa Benin Patrice Talon
Waziri mkuu wa Benin, Lionel Zinzou, amekubali kushindwa na kiongozi wa upinzani katika marudio ya uchaguzi mkuu wa urais nchini humo.
Zinzou, amesema kuwa matokeo ya awali yanaonyesha bayana kuwa Patrice Talon, mfanyibiashara anayefahamika sana kama 'mfalme wa Pamba' atashinda.
Aliyekuwa Rais, Thomas Boni Yayi, hakuwania kiti hicho kwani alikuwa keshaongoza taifa hilo kwa mihula miwili.
Katiba ya Benin haimruhusu tena kuwania muhula wa tatu.
Bwana Talon alirejea kutoka uhamishoni nchini Ufaransa mwaka jana.
Alikimbia Benin baada ya rais kumshutumu kwa kupanga njama ya kumwekea sumu ili afe.
Alikanusha madai hayo.

No comments:

Post a Comment