WATU sita wamekufa na
wengine 38 kujeruhiwa , baadhi yao vibaya, baada ya basi
lenye namba za usajili T 798 AKV mali
ya Lupondije Express Kutoka Mwanza kuja Iringa
kupinduka katikati ya Mteremko wa Mlima Ipogolo
mjini Iringa wakati likielekea stendi ya Ipogolo, kufaulisha abiria waliokuwa
wakielekea mkoani Mbeya.
Imeelezwa
kuwa baadhi ya abiria waliokufa na
majeruhi ni wale ambao walitakiwa kushuka
stendi kuu ya mabasi yaendaye mikoani ya mjini Iringa lakini
hawakushwa kwa kile kilichoelezwa dereva wa basi hilo alikuwa akitaka
kuwawahisha katika basi lingine lililokuwa likiwasubiri setndi ya Ipogolo abiria
waliokuwa wanakwenda Mbeya.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Peter
Kakamba alisema ajali hiyo ilitokea jana (juzi) saa 3:30 usiku baada ya basi hilo
kumshinda dereva na kupinduka.
Kamanda alisema dereva wa basi hilo
Castory Mwalusako (35) alikimbia mara baada ya ajali lakini polisi walifanikiwa
kumkamata.
Mwalusako alisema basi hilo lilimshinda
wakati akishuka mlima kutokana na kupoteza upepo kwenye brek, likapoteza
mwelekeo na kupinduka.
Mganga mkuu wa mkoa wa Iringa Robert
Salim alisema walipokea miili ya watu wanne waliofia katika ajali hiyo huku
wengine wawili wakifariki baada ya kufikishwa hospitali hapo.
Dk Salim alisema waliokukufa ni wanaume
wanne na wanawake wawili, maiti zilizotambuliwa ni mbili Makka Msigwa na Venant
Mhagama aliyefia wodini.
Alisema majeruhi 38 walifikishwa
hospitali ya Iringa ambapo 11 walitibiwa na kuruhusiwa na wengine 27 wamelazwa
wachache wakiwa mahututi.
RPC Kakamba aliwataja waliojeruhiwa
kwenye ajali hiyo kuwa ni Banenda Helen (45) raia wa Kongo, Mbuyi Leoni (52)
raia wa Kongo, Jojina Nyamboko (26) mkazi wa Songea, Magambo Masunga (51)
mkazi wa Mwanza, Felister Mwinuka (19) mkazi wa Njombe, Tubilisiusy
Selestine (33), Said Kitonyi (17), Richard Bett (33) raia wa Kenya na Jofa
Abonga (30)mkazi wa Geita.
Wengine ni Victor Lameck (25), mkazi wa
Kagera, Pius Samwel (20) mkazi wa Mara, Michael Hadu (46) mkazi wa Madaba
Songea, Hassan Mfaume (20) mkazi wa Iringa, Heriet Mwitinda (29) mkazi wa
Arusha, Kiliana Kalinga (22) mkazi wa Mbeya, Hima Kifyasi (32) mkazi wa
Bariadi, Omary Hassan (35) mkazi wa Makambako, Zuo Pawa (30) mkazi wa Mbeya,
Chacha John (26) mkazi wa Iringa.
Wengine Timoth Sichoni (24) mkazi wa
Dodoma, Ishimwe Jasmin (9) rais wa Rwanda, Mkagasana Sarafina (41) rais wa
Rwanda, Zaina Kisaka (26) mkazi wa Manyara, Sara Sichone (26) mkazi wa Mwanza,
Ivon Magaiwa (22)mkazi wa Mafinga, Solomoni Angolisye (58) mkazi wa Dodoma,
Ivan Huwen (33) na mwingine ambaye hajajuliakana jina kutokana na kuwa na hali
mbaya.
Mmoja wa shuhuda wa ajali hiyo James John alisema walitoka Mwanza vizuri na walipofika Iringa dereva alikataa kuwashusha abiria waliokuwa wakiishia Iringa ili awapeleke abiria waliokuwa wakienda mbeya kwenye basi nyingine eneo la Ipogolo.
No comments:
Post a Comment