Serikali imeunda kikosi kazi kinachohusisha taasisi nyeti nchini
kuchunguza sakata la kukamatwa kwa raia wawili wa Uholanzi wakiwa katika
harakati za kusafirisha tumbili 61 kwenda nchini Alb
Kikosi
hicho kinaundwa na maofisa kutoka ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali
(AG), Usalama wa Taifa, Jeshi la Polisi, Uhamiaji na Kikosi cha
Kupambana na Ujangili.
Kamanda wa Polisi Mkoa Kilimanjaro,
Wilbroad Mutafungwa aliwathibitishia wanahabari jana kuundwa kwa kikosi
kazi hicho na kwamba, upelelezi wa sakata hilo umepamba moto.
“Upelelezi
ndiyo kwanza bado mbichi, kwa hiyo siwezi kusema lolote kama lini
watuhumiwa watafikishwa mahakamani kwa sababu upelelezi uko chini ya
kikosi kazi hicho,” alisema Mutafungwa.
Juzi saa tano asubuhi,
Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, alitembelea
Kituo cha Polisi cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia)
kushuhudia wanyama hao.
Profesa Maghembe alisema kama kila kitu
kitakwenda vizuri katika upelelezi, watuhumiwa wa kosa hilo watafikishwa
mahakamani siku ya Jumanne.
Wanyama hao walikamatwa usiku wa
kuamkia juzi katika uwanja huo wakati raia hao, Artem Alik Vardanyian
(52) na Eduard Alik Vardanyian (44) wakiwa katika harakati za
kuwasafirisha kwa kutumia ndege kubwa ya mizigo.
Hata hivyo,
raia hao wa Uholanzi walikuwa na vibali vilivyotolewa na Mkurugenzi wa
Matumizi Endelevu ya Wanyamapori, Charles Mulokozi ambaye tayari
amesimamishwa kazi kwa kashfa hiyo.
No comments:
Post a Comment