Kaimu
Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, David Mnyambuga alisema tukio hilo
lilitokea juzi saa 2.36 usiku katika ofisi za Kampuni ya Simu za Mkononi
ya Halotel, eneo la Medeli.
“Majambazi wapatao saba wakiwa na
mapanga na nondo walifika katika ofisi hizo baada ya kutoboa ukuta na
kumjeruhi askari kwa mapanga na nondo na kupora silaha aina ya SMG,”
alisema.
Kamanda huyo alisema polisi walifanya msako mkali usiku
huo na kufanikiwa kuipata silaha hiyo eneo la Mbuyuni.
“Mtu mmoja
amekamatwa kuhusiana na tukio hilo na anaendelea kuhojiwa,” alisema.
No comments:
Post a Comment