HUKO Recife, Nchini Brazil, katika Mechi ya Kanda ya Marekani ya Kusini ya kuwania kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia, Brazil na Uruguay zilitoka Sare ya Bao 2-2 huku Luis Suarez akicheza Mechi yake ya kwanza tangu afungiwe kwa kung;ata Meno kwenye Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014.
Brazil walitangulia kwa Bao 2-0 na la kwanza likifungwa baada ya Pasi 10 tu toka Mpira uanze na Doglas Costa kuutia Mpira kimiani.
Urugiuay, wakiwa 2-0 nyuma, walipata Bao la kwanza kupitia Edinso Cavani na Luis Suarez kuwasawazishia na kuwapa Sare muhimu ya 2-2.
+++++++++++++++++++
MAGOLI:
BRAZIL 2
-Douglas Costa 1'
-Renato Augusto 26'
URUGUAY 2
-Edinson Cavani 31'
-Luis Suárez 48'
+++++++++++++++++++
Baada ya Mechi 5, Ecuador wanaongoza wakifuata Uruguay, Brazil na Uruguay.
Kundi hili lina Timu 10 na 4 za juu zitafuzu moja kwa moja kwenda Fainali Urusi wakati ile ya 5 itacheza Mechi ya Mchujo ili kufuzu Fainali.
VIKOSI:
Brazil (Mfumo 4-1-4-1): Alisson; Dani Alves, Miranda, David Luiz, Filipe Luis; Luiz Gustavo; Willian, Fernandinho, Renato Augusto, Douglas Costa; Neymar.
Uruguay (Mfumo 4-3-3): Muslera; Fucile, Victorino, Coates, A. Pereira; Sanchez, Arevalo Rios, Vecino; Cavani, Suarez, Rodriguez.
REFA: Nestor Pitana [Argentina]
MSIMAMO:
KOMBE LA DUNIA 2018
Marekani ya Kusini-Mechi za Mchujo
RatibaMatokeo:
**Saa za Bongo
Alhamisi Machi 24
Bolivia 2 Colombia 3
Ecuador 2 Paraguay 2
Chile 1 Argentina 2
Peru 2 Venezuela 2
Jumamosi Machi 26
Brazil 2 Uruguay 2
Jumanne Machi 29
23:30 Colombia v Ecuador
24:00 Argentina v Bolivia
24:00 Paraguay v Brazil
24:00 Venezuela v Chile
24:00 Uruguay v Peru
No comments:
Post a Comment