Siku
chache baada ya Rais wa Zanzibar Dr Ali Mohamed Shein kuapishwa baada
ya kushinda uchaguzi wa marudio uliosusiwa na baadhi ya vyama vya
upinzani, Katibu mkuu wa chama cha wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif
Hamad, amerejea Zanzibar.
Maalim
Seif ambaye alikuwa mapumzikoni katika hoteli ya Serena iliyopo jijini
Dar es Salaam kwa takribani siku 17, jana alirejea Zanzibar kuendelea na
mapumziko yake.
Maalim
Seif alilazwa katika Hospitali ya Hindu Mandal ya jijini Dar es
Salaam,mara baada ya kuruhusiwa March 8 mwaka huu alishauriwa na Daktari
wake kupata mapumziko ya muda mrefu.
Kurejea
kwa Maalim Seif visiwani humo kunazidisha shauku na kiu ya baadhi ya
Wazanzibar kutaka kusikia atakachokisema kiongozi huyo wa upinzani
mwenye ushawishi mkubwa kwenye jamii.
Maalim
Seif aliugua wakati Wazanzibar wakiwa katika maandalizi ya kurudia
uchaguzi mkuu uliofanyika March 20, mwaka huu baada ya kufutwa kwa
matokeo ya uchaguzi uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana na mwenyekiti wa
tume ya uchaguzi ya Zanzibar( ZEC), Jecha Salim Jecha kwa madai kuwa
uligubikwa na dosari nyingi.
Gharama za Hotelini
Taarifa
zilizoripotiwa kwenye vyombo vya habari siku chache zilizopita zilidai
kuwa kila siku aliyokaa kwenye hoteli hiyo, Maalim Seif alikuwa akitumia
wastani wa Sh. 6,162,500.
Kutokana na takwimu hizo, hadi kufikia jana, Maalim Seif atakuwa ametumia kiasi kisichopungua sh. Milioni 92.4
Chumba
alichokuwa akilala Maalim Seif katika Hoteli hiyo yenye hadhi ya nyota
tano kinalipiwa dola za Marekani 2,500 kwa usiku mmoja.
Maalim
Seif alikuwa akiishi hotelini hapo na wasaidizi wake watano, ambao wote
gharama zao zinalipwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ)
No comments:
Post a Comment