RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed
Shein leo amemuapisha Bwana Said Hassan Said, kuwa Mwanasheria Mkuu wa
Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyeikiti wa Baraza la Mapinduzi alimteua Bwana Said Hassan jana kushika wadhifa huo kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu cha 55 (1) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
Hafla
ya kumuapisha Mwanasheria Mkuu huyo ilifanyika Ikulu Mjini Zanzibar na
kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar.
Miongoni
mwao ni Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu, Katibu Mkuu
Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee,
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Abdalla Mwinyi Khamis.
Wengine
ni Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali, Naibu
Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Mahmoud Mussa Wadi, Meya wa Manispaa ya
Mji wa Zanzibar Khatib Abrahman Khatib,Washauri wa Rais wa Zanzibar na
viongozi wengine wa Serikali.
Viongozi
mbali mbali na watendaji waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Said
Hassan Said kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar katika ukumbi wa mikutano
Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi.
No comments:
Post a Comment