Monday, 21 March 2016

Sababu 4 Kwanini Madrid Wanataka kumuuza James Rodriguez



Kwa mara ya 3 mfululizo, James Rodriguez alizomewa na mashabiki wake wa Real Madrid. Mshambuliaji huyo wa Colombia alijikuta kwenye jicho la tatu la mashabiki wa Santiago Bernabeu, kila alipogusa mpira alizomewa na mashabiki.
 James amekuwa na msimu mbaya  – jambo ambalo limepelekea sio mashabiki tu wa Real kutoridhishwa na kiwango chake bali pia viongozi wa klabu. Imefikia mpaka sasa anatajwa kuwa miongoni mwa wachezaji watakaouzwa. Lakini nini kimemtokea mchezaji huyu aliyekuwa kipenzi cha Madrid wakati akisajiliwa? Hizi hapa sababu 4 kwanini James anataka kuuzwa na Madrid..
  1. Kushuka Kiwango
Sababu kubwa ya Madrid wanahitaji kumuondoa kwenye kitabu cha mishahara ni kutokana na kushuka kiwango ukilinganisha na msimu uliopita. Amecheza mechi 22 na kufunga magoli 6 msimu huu, wakati msimu wa  2014-15  alicheza mechi 46 na kufunga magoli 17. Amekuwa akiongeza tatizo kwa kushindwa kufiti katika mfumo wa 4-3-3 ambao ulitambulishwa na Rafa Benitez, na sasa unatumiwa na Zinedine Zidane.
  2. Matukio ya Nje ya Uwanja
Maisha binafsi ya mcolombia huyo yamekuwa yakitawala vichwa vya habari vya magazeti ya Hispania. Siku ya mkesha wa mwaka mpya alikamatwa akiendesha spidi kilomita 200 kwa sasa wakati akienda mazoezini na bado  akagoma kusimama aliposimamishwa na Polisi. Baada ya suala hilo kutolewa kwenye vyombo vya habari – Rodríguez alijitetea kwanba alishindwa kusimama kwa sababu alihisi waliokuwa wakimkimbiza walikuwa wahalifu waliotaka kumteka. Tabia nyingine inayowachukiza Madrid nikukesha usiku kwenye vilabu vya usiku.
  3. Ombi la kuongezewa Mshahara
Miezi michache iliyopita, wakala wa James, Jorge Mendes, alijaribu kuwasiliana na mabosi wa Bernabeu ili kuomba mteja wake aongezewe mshahara wake. Ombi hilo limewakera mabosi hao ukizingatia kiwango cha chini  alichonacho sasa.
  4. Thamani Kubwa Sokoni
Pamojana matatizo aliyonayo ndani na nje ya uwanja, mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24 bado anachukuliwa kuwa mmoja wa wachezaji wenye thamani kubwa sokoni. Anatajwa kuwa na thamani ya 80 million euros. Inaripotiwa, Pep Guardiola ni shabiki wa mchezaji huyo na huenda akamsaji huyo wakati atakapohamia Man City. Man United na Chelsea pia zinatajwa kuvutiwa na Mclombia huyo.

No comments:

Post a Comment