Monday, 21 March 2016

Cech mchezaji bora wa mwaka

Image result for Czech Petr Cech

Golikipa wa kimataifa ya Jamuhuri ya Czech Peter Cech ametangazwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa nchi hiyo.
Cech Mwenye umri wa miaka 33,alichaguliwa na makocha, wachezaji na viongozi wa timu kutwaa tuzo ya nane ya uchezaji bora nchini mwake.
Golikipa huyu amewazidi wachezaji wenzake wa timu ya taifa Mshambuliaji wa Sparta Prague David Lafata, na kiungo wa Vladimir Darida anayeichezea Hertha Berlin.
kipa huyu wa klabu ya Soka ya Arsenal ameichezea timu ya taifa michezo 118 tangu alipoanza soka la kimataifa mwaka 2002.

No comments:

Post a Comment