Monday, 21 March 2016

MAYANJA AENDELEA KUWANYOOSHA WACHEZAJI WA SIMBA, SAFARI HII NI BANDA

Adbi Banda akiwaungia mkono mashabiki wa Simba mara bada ya kutolewa nje ya mchezo kwa kadi nyekundu na mwamuzi Jonesi Rukyaa kufuatia kuoneshwa kadi mbili za njano
Adbi Banda akiwaungia mkono mashabiki wa Simba mara bada ya kutolewa nje ya mchezo kwa kadi nyekundu na mwamuzi Jonesi Rukyaa kufuatia kuoneshwa kadi mbili za njano kwenye mchezo wao dhidi ya Ynga February 20 mwaka huu
Kocha mkuu wa Simba Jackson Mayanja anasema amesikitishwa na kitendo cha mchezaji wake Abdi Banda kugoma kupasha ili kuingia kucheza wakati Simba ilipocheza na Coastal Union siku ya Jumamosi kwenye uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
“Mchezaji anakaa benchi unamwambia ajiandae kuingia uwanjani, anakataa akihoji kwanini anakaa benchi”.
“Mimi kama kocha wa Simba siwezi kukubali mchezaji yeyote ambaye hana nidhamu. Hakuna mchezaji ambaye yupo juu ya klabu hata kama ni klabu ya Sinza, kama ina uongozi na waalimu”.
“Mimi sitaki mchezaji ambaye hana nidhamu, iyo ndiyo kanuni kama kuna kocha yeyote Tanzania ambaye anataka kuchezesha watu ambao hawana nidhamu hafanyi kazi. Aafikiri yupo juu ya kocha au wachezaji wenzake”.
Hivi karibuni uongozi wa klabu ya Simba ulimsimamisha Hassan Isihaka ikiwa pamoja na kumvua jukumu la unahodha msaidizi kwasababu ya kumtolea maneno makali Mayanja kutokana na kuwekwa benchi kwa muda mrefu.
Tangu Banda atolewe nje kwa kadi nyekundu kwenye mchezo kati ya Simba dhidi ya Yanga uliochezwa February 20 mwaka huu kwenye uwanja wa taifa, mchezo uliomalizika kwa Simba kufungwa magoli 2-0.

No comments:

Post a Comment