Amekuwa
mchezaji wa kwanza wa Spurs katika kipindi cha miaka 44 kufunga magoli
20 au zaidi katika misimu miwili mfululizo. Shujaa wa Tottenham Martin
Chivers alifunga magoli 21 ya ligi katika msimu wa 1970-71 na akafunga
magoli 25 msimu uliofuatia.
Na Harry Kane amefuata nyayo zake kwa magoli mawili aliyofunga dhidi ya Bournemouth @White Hart Lane ambayo yamefanya atimize magoli 21, idadi sawa na ya msimu uliopita.
Kane alisema: Nina furaha sana na ushindi wa 3-0, ushindi mzuri kuelekea break ya mechi za kimataifa.”
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa England sasa anaungana na listi ya wachezaji wa Uingereza ambao waliweka rekodi kama yake. Kane ndio mchezaji wa kwanza wa England tangu Alan Shearer mwaka 1997 kufunga magoli 20 au zaidi kwa misimu miwili mfululizo.
Harry Kane anakuwa mchezaji wa tano wa England katika historia ya
Premier League Shearer, Robbie Fowler, Les Ferdinand na Andy Cole kuwa
na rekodi ya kufunga magoli 20 au zaidi katika misimu miwili mfululizo.
No comments:
Post a Comment