Saturday, 26 March 2016

Ronaldo ashindwa na penalti

Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo alikosa penalti kwa mara ya pili mfululizo huku timu yake Portugal ikipoteza nyumbani dhidi ya Bulgaria katika mechi ya kirafiki.
Marcelinho alifunga bao lake la kwanza na hivyobasi kuwapatia wageni hao uongozi katika kipindi cha kwanza alipofunga kupita pasi nzuri.
Portugal ilitawala mechi hiyo lakini mlinzi wa Bulgaria Leiria alikataa katakata kuwapisha washambuliaji wa Ureno.
Ronaldo ambaye alikosa penalti akiichezea Real Madrid dhidi ya Sevilla siku ya jumapili aliona mkwaju wake wa kipindi cha pili ukiokolewa baada ya Nikolay Boduro wa Bulgaria kuunawa mpira katika eneo la hatari.
Hatahivyo licha ya kushindwa kufunga penalti hiyo dhidi ya Sevila Real Madrid iliibomoa Sevilla mabao 4-0 katika mechi ya La Liga lakini penalti dhidi ya Bulgaria ilikuwa mwiba kwa Portugal kwa kuwa licha ya kushambulia mara 30 hawakuweza kufunga.

No comments:

Post a Comment